Na wasamalia wema
Kijana mwingine apigwa na kuchomwachomwa visu mwilini mwake na kundi la watu maeneo ya makaburi ya don bosco barabara ndogo inayoelekea mkwawa(iringa manispaa) saa 2 usiku.kundi hili la watu lilimyang'anya simu na pesa tsh 15,000/- tarehe 12/09/2013.Hili ni tukio lingine baada ya lile la kijana aliyenyofolewa macho maeneo karibu na eneo hilihili la makaburi tarehe 08/09/2013.Sasa eneo linalozunguka makaburi haya limekuwa ni tishio kwa watu wanaopita maeneo hayo hasa wakati kuanzia saa 1 jioni na kuendelea.waliotoa taarifa hizi wanasema lengo la vibaka hawa ni vitu vidigovidogo kama pesa na simu.
No comments:
Post a Comment